Washukiwa wawili wa wizi wa mabavu wakamatwa Kisumu

Martin Mwanje
1 Min Read
Washukiwa wa wizi waliokamatwa Kisumu

Hatimaye siku 40 zilitimia kufuatia kukamatwa kwa washukiwa wawili sugu wa wizi wa mabavu katika kaunti ya Kisumu.

Wawili hao wamekuwa wakisakwa na polisi kwa muda.

Kwa mujibu wa Idara ya Taifa ya Polisi, NPS, washukiwa hao walikamatwa kufuatia operesheni iliyofanywa na maafisa wa polisi waliokuwa na taarifa za kijasusi.

Maafisa hao walivamia nyumba moja katika eneo la Kanyametha huko Obunga, katika kaunti ndogo ya Kisumu Central walikojificha washukiwa hao.

Upekuzi mkali uliofanywa kwenye nyumba hiyo ulibaini uwepo wa vitu kadhaa vinavyoaminika kuibwa.

NPS imetaja kukatwa kwa wawili hao kama ushindi katika juhudi za kukomesha uhalifu katika eneo hilo huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Share This Article