Maeneo kadhaa kukosa umeme leo

Marion Bosire
2 Min Read
Baadhi ya kaunti hapa nchini kukosa nguvu za umeme.

Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya Power imetangaza maeneo mbali mbali nchini ambayo yatakosa huduma za umeme leo Ijumaa Septemba 19, 2025.

Kenya Power ilitaja maeneo yaliyo kwenye kaunti nne, Nairobi, Murang’a, Nyeri na Kisumu, ambayo yatakosa umeme kwa hadi saa tisa leo ili kutoa fursa ya ukarabati wa vifaa vya umeme katika maeneo hayo.

Wahandisi wa kampuni hiyo watakuwa wakiweka vifaa vya teknolojia ya kisasa huku wakiondoa mitambo ya transformer iliyoharibika au kuchakaa na kuweka mingine mipya.

Katika kaunti ya Nairobi maeneo yatakayokosa umeme ni pamoja na Thome, Mirema Road, Mirema Drive, Thome 1, USIU, TRM Drive, Safari Park Gardens na maeneo ya karbu.

Huko Murang’a maeneo yatakayokosa huduma za umeme leo ni makao ya watoto ya Kandara, maeneo ya chini ya mji wa Kandara, Githuya, Gatundu, Kiriko-Ini, shule ya msingi ya Kandara, makanisa ya Kiriko-Ini PCEA na Catholic, Sunset, Father Murichu’s na mengine ya karibu.

Katika kaunti ya Nyeri maeneo haya hayatakuwa na umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, Mathari Nyewasco Water Tank, shule ya St. Teresa na maeneo ya karibu.

Maeneo mengine ni shule ya upili ya Wandumbi, soko la Wandumbi, DW Nderitu, Kamahuru TBC na mengine yaliyo karibu.

Hko Kisumu hakutakuwa na umeme katika eneo la soko la Ogilo, Obagu, soko la Masogo, lile la Ombeyi, Onyalo Biro, Miwani na mengine ya karibu.

Share This Article