Mwanamuziki wa Marekani Cardi B amefichua kwamba yeye na mpenzi wake Stefon Diggs wanatarajia mtoto.
Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy alifichua kwamba ana ujauzito wa mchezaji huyo wa mpira wa miguu kwenye mahojiano na Gayle King kwenye kipindi kiitwacho ‘CBS Mornings’ Jumatano.
“Ninajihisi mwenye nguvu, ninajihisi mwenye uwezo, kwamba ninafanya kazi hizi zote, lakini ninafanya kazi hizi nikiwa natengeneza mtoto” alisema Cardi B.
Mtoto huyo anayetarajiwa atakuwa wake wa nne na wa kwanza kwa Diggs kwani Cardi B tayari ana watoto wengine watatu aliopata na mwanamuziki Offset.
Uvumi kuhusu ujauzito huo ulikuwa umesambaa mitandaoni kwa wiki kadhaa kabla yake kutangaza jana. Alifichua pia kwamba mtoto huyo atazaliwa kabla ya ziara yake ya Februari mwakani.