Nepal yatoa fidia ya shilingi milioni 1.3 kwa kila familia ya Gen Z aliyeuawa

Dismas Otuke
1 Min Read

Kila familia ya Gen Z aliyeuawa kwa maandamano nchini Nepal italipwa fidia ya shilingi milioni 1.3 za Kenya, sawa na Rupia milioni 1.5.

Taarifa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Nepal Om Prakash, ilisema fedha hizo zitaanza kugawanywa kwa familia za wafiwa kuanzia leo Septemba 18 kupitia ofisi za Wilaya baada ya kumalizika maombolezo ya kitaifa leo hapo jana.

Tangazo hilo linajiri wiki chache baada ya vijana wa Gen Z 72 kuuawa kwenye maandamano ya kupinga ufisadi serikalini uliochangia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Sharma Oli.

Aliyekuwa Jaji Mkuu Shushila Karki aliteuliwa kuwa Kaimu Waziri Mkuu baada ya GenZ nchini humo kupendekeza kuteuliwa kwake.

Share This Article