Huku wingu la kisiasa la uchaguzi mkuu ujao likianza kutanda nchini, jamii ya Iteso katika Kaunti ya Trans Nzoia imeweka mikakati inayodhamiria kuimarisha umoja wao kwenye uchaguzi huo ili iweze kunufaika serikalini.
Katika mkutano uliofanyika mjini Kitale, jamii hiyo ilichagua viongozi 25 watakaoiwakilisha katika wadi zote za kaunti ya Trans Nzoia na mmoja katika ngazi ya kaunti kama msemaji wake.
Jamii hiyo Sasa inasema ni wakati muafaka wa kutambulika na kupewa nafasi mbalimbali za uongozi bila kubaguliwa na kuhakikisha kuwa mwafaka wa Mabanga unazingatiwa kikamilifu kuwahakikishia keki ya uongozi.
Kadhalika, viongozi hao wamedokeza kumteua mbunge wa Teso Kaskazini Edward Oku Kaunya kuwa msemaji wake nchini huku wakimtwika majukuma ya kuwakilisha jamii hiyo yana ya Iteso Ateker yaani Iteso na Turkana katika meza ya kitaifa.