Mshukiwa wa wizi wa kazi za Beyonce akamatwa

Marion Bosire
1 Min Read

Maafisa wa polisi huko Atlanta wamekamata mshukiwa wa wizi wa kazi za muziki za Beyonce ambazo hazikuwa zimezinduliwa rasmi.

Kelvin Evans alikamatwa kwa makosa ya kuvunja gari aina ya SUV miezi miwili iliyopita na kuiba vitu vya thamani vya msanii huyo maarufu.

Mwezi Julai polisi hao walijibu wito wa tukio hilo la wizi na walipofika, wahudumu wawili wa kundi la Beyonce ambao ni mwalimu wa densi na mcheza densi waliwaarifu kwamba kio cha dirisha ya nyuma ya gari hilo kilivunjwa na wahudika waaondoka na mabegi mawili.

Kulingana na polisi, hifadhi ya miziki hiyo mipya, orodha za vifaa vya jukwaani na mipango ya unakili wa picha na video kwa ajili ya ziara ya “Cowboy Carter” ndivyo vitu vilikuwa kwenye mabegi yaliyoibwa.

Evans anashikiliwa katika jela ya Fulton County na polisi hawajapata vitu anavyodaiwa kuiba hadi sasa.

Share This Article