Jaji wa Mahakama ya Rufaa Fredrick Ochieng Andago ameaga dunia.
Hata hivyo, kwenye taarifa, Idara ya Mahakama haijaeleza kilichosababisha kifo cha Jaji huyo aliyejiunga na idara hiyo mnamo mwaka 2003, wakati huo kama Jaji wa Mahakama Kuu.
Alipandishwa ngazi na kuwa Jaji katika Mahakama ya Rufaa mwaka 2022.
“Atakumbukwa kama mweledi katika uendelezaji wa sheria ya biashara nchini Kenya na kama mpiganiaji wa ukuzaji wa utatuzi mbadala wa migogoro,” alisema Jaji Mkuu Martha Koome kwenye taarifa.
“Wakati wa kifo chake, alikuwa akihudumu kama mwenyekiti wa Jopo la Upatanishi la Mahakama, ambalo linasimamia uanzishwaji wa Upatanishaji Nje ya Mahakama.”
Jaji Andago aliwahi kuhudumu kama jaji katika vituo vya Kakamega, Kitale na Kisumu.