Upigaji kura wakamilika nchini Malawi

Dismas Otuke
1 Min Read

Upigaji kura nchini Malawi imefungwa rasmi leo jioni huku vituo vyote vya kupigia kura vikifungwa saa kumi na moja.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Malawi, Jaji Annabel Mtalimanja, ameelezea kuridhishwa kwake na idadi ya wapiga kura iliyojitokeza leo kutekeleza haki yao ya kidemokrasia.

Upigaji kura huo ulijumuisha viongozi wa serikali za mitaa, wabunge, na rais.

Kinyang’anyiro cha Urais ni kinawashirikisha wagombeaji 17.

Hata hivyo kivumbi cha Ikulu ni kati ya Rais wa sasa Lazarus Chakwera aliye na umri wa miaka 70 wa chama cha Malawi Congress (MCP), dhidi ya aliyekuwa rais Peter Mutharika wa chama cha Democratic Progressive (DPP), aliye na umri wa miaka 85.

Jumla ya wapiga kura milioni 7.2 walijiandikisha kwa uchaguzi huo mkuu huku mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais akihitaji zaidi ya asilimia 50 ili kutangazwa mshindi.

Aidha, Wabunge 299 na madiwani 509 watachaguliwa huku matokeo hayo yakitarajiwa kufikia Septemba 30.

Share This Article