Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune siku ya Jumapili alimteua Sifi Ghrieb, kuwa Waziri Mkuu mpya akijukumiwa kubuni serikali mpya.
Sifi anatwaa nafasi iliyoachwa wazi na Nadir Larbaoui, aliyepigwa kalamu Alhamisi iliyopita baada ya kuhudumu tangu Novemba mwaka jana.
Hata hivyo serikali haikutoa sababu zozote za kutimuliwa kwa Nadir.