Makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani yameratibiwa kuandaliwa baina ya Septemba 13 na 21 mwaka huu mjini Tokyo,Japan.
Jumla ya wanariadha 2,000 kutoka mataifa 200 wanatarajiwa kushiriki ,Kenya ikiwakilishwa na kikosi cha wanariadha 58.
Kenya itakuwa ikitetea mataji ya mita 1500 wanawake na mita 5,000 kupitia kwa Faith Kipyegon na Mary Moraa katika mita 800.
Aidha,kwa mara ya kwanza Kenya itawakilishwa kwa mara ya kwanza katika shindano la urushaji sagai kwa wanawake kupitia kwa Irene Jepkemboi.
Mashindano hayo yataanza Jumamosi hii huku fainali ya kwanza kwa Wakenya ikiwa mita 10,000 wanawake saa tisa unusu alasiri ambapo bingwa wa dhahabu mbili za Olimpiki Beatrice Chebet atawaongoza wenzake Agnes Jebet Ng’etich na Janeth Jepng’etich