Wakili Mathew Kyalo Mbobu auawa kwa kupigwa risasi

Maafisa wa ujasusi wameanzisha uchunguzi kubaini kiini na wahusika wa mauaji hayo ya kinyama.

Dismas Otuke
0 Min Read

Wakili maarufu katika kaunti ya Nairobi Mathew Kyalo Mbobu amefariki. 

Mbobu alipigwa risasi na kuuawa papo hapo na watu wasiojulikana jana Jumanne jioni.

Alikumbana na mauti akiwa kwenye gari lake mtaani Karen.

Maafisa wa ujasusi wameanzisha uchunguzi kubaini kiini na wahusika wa mauaji hayo ya kinyama.

Visa vya watu kupigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana vimeongezeka nchini katika siku za hivi karibuni.

Share This Article