Wazazi waua mwanao kwa tuhuma za wizi Tanzania

Marion Bosire
1 Min Read

Raia wa Tanzania wameshangazwa na kisa ambapo wazazi wawili waliua mwanao wa kiume kwa tuhuma za wizi katika kata ya Iganzo, wilaya ya Mbeya nchini Tanzania.

Kisa hicho kinahusisha mwendazake mtoto Bright Joel Malila, ambaye anaripotiwa kupatiwa kipigo na wazazi wake Bwana Joel Malila na mkewe wakimtuhumu kuiba runinga ya nyumbani kwao na kisha kutokomea kusikojulikana.

Majirani wa Bwana Joel Malila wamesema siku ya tukio walisikia kelele wazazi wakimwadhibu mtoto huyo, kelele ambazo zilisikika kwa muda mfupi sana .

Majirani hao walidhania kwamba ni hali ya kawaida kwa mzazi kufanya hivyo lakini baadaye waliitwa na kushtushwa na kile walichokiona.

Mashahidi wanasema walipoingia ndani walikuta mtoto akiwa chini na hali mbaya na wakafanya mpango wa haraka wa kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitali ambapo muda mfupi baadaye walipatiwa taarifa za kwamba mtoto huyo amefariki.

Afisa wa polisi wa kata ya Iganzo Alex Mwalukasa sasa anahimiza wananchi wa kata hiyo kutoa taarifa mapema pindi wanapoona dalili za ukatili ili kuzuia matukio kama hayo.

Mwakilishi wa serikali katika huku mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa igodima akiwaomba wananchi hao kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi.

Share This Article