Gavan Achani apiga jeki juhudi za kumaliza uhaba wa maji Kwale

Dismas Otuke
1 Min Read

Katika juhudi za kukabiliana na uhaba wa maji Gavana wa Kwale Fatuma Achani amefungua visima viwili vya maji safi vya Ibn Sina na Mwangoloko, kwa Kizuka huko Kinondo eneo la Msambweni .

Visima hivyo vitawasaidia wakaazi zaidi ya 600 wa vijijini hivyo ambao wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kutafuta maji safi.

Kaunti ya Kwale imechimba mabwawa ya maji zaidi ya 50, katika maeneo ya LungaLunga,Kinango na Samburu, visima zaidi ya 60 ,katika magatuzi madogo ya Matuga na Msambweni na kuunganisha na kupanua mabomba ya maji kwa zaidi ya kilomita 500, ili kukabiliana na uhaba wa maji hasa maeneo kame ya Kaunti hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Achani ameahidi kutatua swala la uhaba wa maji liliokithiri kwa muda mrefu akidokeza kushirikiana na washikadau mbalimbali kuhakikisha Mkwale anapata maji safi.

Share This Article