Ruto awaaga wanariadha wa Kenya wanaoelekea Tokyo

Kenya italenga kuboresha matokeo ya mwaka 2023 mjini Budapest ilipotwaa dhahabu 3, fedha 3 na shaba nne.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto jana Jumatano usiku aliikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya Kenya itakayoshiriki makala ya 20 ya mashindano ya riadha ulimwenguni kuanzia wiki ijayo jijini Tokyo nchini Japani.

Alikariri kujitolea kwa serikali kuwaunga kuwaunga mkono wanariadha ili wasajili matokeo bora.

Wanariadha Zaidi wataiwakilisha Kenya katika makala ya mwaka huu yatakayoanza tarehe 13 mwezi huu hadi tarehe 21.

Kenya italenga kuboresha matokeo ya mwaka 2023 mjini Budapest ilipotwaa dhhabu 3, fedha 3 na shaba nne.

Faith Kipyegon na Mary Moraa watakuwa wakitetea mataji waliyotwaa miaka miwili iliyopita.

Share This Article