Morocco watwaa Kombe la CHAN kwa mara ya tatu

Kombe hilo lilikuwa la tatu kwa jumla kwa Morocco, ambao pia walitawazwa mabingwa mwaka 2018 na 2020 na kuwa timu ya kwanza kushinda mataji matatu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Morocco almaarufu Atlas Lions ndio mabingwa wa soka barani Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN baada ya kuwacharaza Madagascar, kwenye fainali ya kukata na shoka iliyosakatwa katika uchanjaa wa kimataifa wa Kasarani Jumamosi jioni.

Kombe hilo lilikuwa la tatu kwa jumla kwa Morocco, ambao pia walitawazwa mabingwa mwaka 2018 na 2020 na kuwa timu ya kwanza kushinda mataji matatu.

Madagascar walichukua uongozi dakika ya 9 kupitia kwa Felicite Manohantsoa, aliyefyatua tobwe kabla ya Khalid Baba kukomboa dakika ya 27.

Mfungaji bora Oussama Lamlioui aliwawaweka Simba wa Milima ya Atlas kwa uongozi wa 2-1 kufikia mapumziko.

Toky Rakotondraibe alisawazisha kwa Madagascar dakika ya 68.

Hata hivyo Lamlioui alipachika bao maridadi kutoka karibu katikati ya uwanja zikisalia dakika 10 mchezo ukamilike na kuwahakikishia Morocco ushindi.

Kiungo wa Morocco Mohammed Hrimat alitangazwa mchezaji bora wa kipute hicho.

Kenya ,Uganda na Tanzania zilishirikiana kuandaa dimba hilo lililokuwa na timu 19 kwa mara ya wkanza.

Rais wa shirikisho la soka Duniani Gianni Infantino, mwenzake wa shirikisho la kandanda Afrika Dkt Patrice Motsepe na Rais William Ruto walikuwa baadhi ya watu wenye hadhi walioshuhudia mechi hiyo.

Pambano hilo lilitanguliwa na sherehe za kufunga mashindano.

 

Share This Article