Kenya kupanua ushirikiano wa Leba na Uingereza

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Kenya inapania kupanua ushirikiano wa mwafaka wa Leba kati yake na Uingereza, ili kuwashirikisha maafisa wa matibabu na madaktari.

Katibu katika Wizara ya Leba na Makuzi ya Ujuzi Shadrack Mwadime, alisema haya jana alipohutubia kikao cha tano cha kimataifa cha maafisa wa afya na chama cha madaktari -GACOPA, katika chuo kikuu cha Aston mjini Birmingham, Uingereza.

Alisema hatua hiyo italinda utambuzi wa taaluma na usafiri wa wafanyikazi pamoja na kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya wahudumu wa afya.

Aidha, aliongeza kuwa serikali ya Kenya inashirikiana na mataifa ya Uingereza na Ireland Kaskazini ili kuwa na mfumo bora wa uhamiaji wa wafanyikazi kati ya nchi hizo.

Kongamano hilo linawaleta pamoja wajumbe 74 wa GACOPA kutoka mabara ya Ulaya, Afrika, Asia, na Marekani ili kuongoza utambuzi wa ujuzi.

Ujumbe wa Kenya kwenye kongamano hilo unajumuisha Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu afya.

Patrick Munene na kamati ya and National Chairman for the Kenya Clinical Officers Association (KCOA), Peterson Wachira.

Share This Article