Rais William Ruto ameapa kuwachukulia adhabu kali wale wote watakaopatikana na hatia kupora pesa za hazina ya afya SHA.
Ruto aliyekuwa akizungumza jana katika Ikulu ya Nairobi alipokutana na viongozi wa mashinani kutoka kaunti ya Kiambu, alisema hospitali na watu binafsi watakaopatikana kuhusika kwa uporaji wa pesa hizo wataadhibiwa kisheria.
Matamshi yake yanajiri wakati ambapo Wabunge wamemfokea waziri wa Afya Aden Duale, kutokana na ufisadi uliokithiri katika hazina ya SHA wakiapa kumngátua au ajiuzulu .
Hospitali,zahanati na vituo kadhaa vya afya tayari vimepigwa marufuku kwa kuhusika katika njama ya kughushi malipo ya matibabu.