Timu ya taifa ya Voliboli ya wanawake ya Kenya Malkia Striker, ilisajili ushindi wa kwanza katika mechi ya mwisho ya mashindano ya Dunia yanayoendelea nchini Thailand.
Kenya waliicharaza Vietnam leo seti 3-0 za 25-23, 25-22 na 25-18 ukiwa shindi wa tatu katika historia tangu waanze kucheza mashindano ya Dunia.
Malkia Strikers walikuwa wamepoteza mechi mbili za awali kundi G seti 3-0 na 3-1 dhidi ya Ujerumani na Poland mtawalia.