Kennedy Rapudo ambaye ni mfanyabiashara jijini Nairobi amezima uvumi uliokuwa ukienezwa mitandaoni kwamba yeye na mke wake Amber Ray wametengana.
Uvumi huo ulitokana na hatua ya Rapudo ya kukosa kuonekana kwenye video za mitandaoni za Amber kinyume na mazoea kiasi kwamba walikuwa wamekuwa familia maarufu mitandaoni pamoja na binti yao Africana.
Rapudo alizungumzia suala hili kwenye mahojiano ambapo hakukubali au kukataa kuachana na mkewe na badala yake akasisitiza kwamba mambo ya familia yao ni ya faragha na sio ya mitandaoni.
“Nimesema kwamba tumetengana? Umemsikia Amber akisema tumeachana? Iwapo tungeachana habari zingetoka kwanu ama kwake. Kwa sasa acha watu waongee” alijibu Rapudo.
Hatua ya Amber ya kuonyesha ukarabati wa nyumba yao mitandaoni na kuuza baadhi ya samani mitandaoni iliongeza kasi ya uvumi huo wengi wakiamini kwamba Rapudo amegura ndiposa fanicha za afisi yake ya nyumbani zinauzwa.
Kuhusu madai ya kupoteza uzani wa mwili kutokana na kuvunjika kwa ndoa yake, Rapudo alikanusha akisema aliamua kupunguza mwili wake kutokana na sababu za kiafya hususan shindikizo la damu.
Mwanao Africana, Rapudo alisema anafahamu aliko na yuko sawa ishara kwamba uhusiano kati yake na Amber Ray bado uko imara.
Haya yanajiri siku chache baada ya picha kusambaa mitandaoni ikimwonyesha Rapudo na mwanamke mwingine aliyedai kwamba Rapudo alikuwa amempeleka sehemu kubarizi.
Lakini Rapudo alijitetea na kukanusha madai hayo akifafanua kwamba alisaidia wanawake fulani kuegesha gari lao baadaye wakaomba kupiga picha naye.