Bingwa wa Jumuiya ya Madola katika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala amejiondoa kushiriki fainali ya Diamond League mjini Zurich, Uswizi, kati ya tarehe 27 na 28 mwezi huu kutokana na jeraha.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Omanyala, ambaye mazoezini mjini Miramas nchini Ufaransa, amesema jeraha la nyonga alilo nalo halijapona.
Aidha Omanyala amesema anatarajia jeraha hilo kupona kwa wakati ili ashiriki mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo, Japan.