Takwimu muhimu za CHAN baada ya robo fainali

Magoli 80 yamefungwa huku mshambulizi wa Morocco Oussama Lamlioui, anaongoza kwa kupachika magoli manne kufikia sasa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya mechi 40 kati ya 44 zimesakatwa tangu kuanza kwa makala ya nane ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa nyumbani CHAN zinazoandaliwa kwa pamoja na Kenya,Uganda na Tanzania.

Magoli 80 yamefungwa huku mshambulizi wa Morocco Oussama Lamlioui, anaongoza kwa kupachika magoli manne kufikia sasa.

Wanandinga wengine watatu wamefumania nyavu mara tatu kila mmoja wakiwemo;Thabiso Kutumela wa Afrika Kusini,Soufiane Bayazid wa Algeria na Allan Okelo wa Uganda.

Mechi za nusu fainali zitaandaliwa Jumanne Agosti 26,  Sudan wakifungua dimba dhidi ya Madagascar saa kumi na moja jioni, jijini Kampala ,kabla ya mabingwa watetezi Senegal  kumaliza udhia na mabingwa

mara mbili Morocco  jijini Dar es Salaam.

Share This Article