Tanzania  waishiwa pawa nyumbani dhidi ya Morocco

Taifa Stars wanajiunga na waandalizi wenza Kenya ambao pia walifurushwa katika makala ya mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa fainali za CHAN mwaka huu, Tanzania almaarufu Taifa Stars, waliaaga kipute hicho baada ya kuzidiwa maarifa walipozabwa goli moja kwa nunge na Morocco katika robo fainali jana usiku.

Timu zote zilitoka sare tasa kunako kipindi cha kwanza kabla ya Simba wa Atla kupata goli la ufunguzi dakika ya 65, kupitia kwa Ousama Lamlioui akiunganisha pasi ya Youssef Belammari.

Licha ya kutopoteza mechi katika hatua ya makundi, Tanzania walishindwa kwa mara ya kwanza na kuyaaga mashindano.

Taifa Stars wanajiunga na waandalizi wenza Kenya ambao pia walifurushwa katika makala ya mwaka huu.

 

Share This Article