Lumngole atwaa ushindi wa kwanza Diamond League

Lemngole aliye na umri wa miaka 23 aliziparakasa mbio hizo kwa dakika 9 sekunde 16.36.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chipukizi wa Kenya mwenye makao yake nchini Marekani, Dorris Lemngole, alitwaa ushindi wa kwanza wa Diamond League aliposhinda mita 3000 kuruka viunzi na maji katika mkondo wa Lausanne, Uswizi jana usiku.

Lemngole aliye na umri wa miaka 23 aliziparakasa mbio hizo kwa dakika 9 sekunde 16.36.

Chipukizi huyo ambaye pia amefuzu kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya dunia mwezi ujao mjini Tokyo, Japani, kwa mara ya kwanza, aliwashinda mibabe kama vile Sembo Almayew wa Ethiopia, aliyemaliza wa pili kwa dakika 9 sekunde 20.39.

Olivia Markezich, a Marekani, alimaliza wa tatu kwa dakika 9 sekunde 20.73.

Bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi alizidiwa maarifa katika mita 800, akimaliza wa pili kwa dakika 1 sekunde 43.29.

Hosh Joey wa Marekani aliibuka mshindi kwa kuzitimka kwa dakika 1 sekunde 42.82, naye Mohammed Attaoui wa Uhispania akaridhia nafasi ya tatu.

Share This Article