JOBO na Musingu kumenyana kwenye nusu fainali

Hii ni baada ya timu hizo kumaliza za kwanza na pili mtawalia kwenye makundi yao.

Marion Bosire
1 Min Read

Shule za St.Joseph (JOBO) na Musingu zitamenyana tena hapo kesho katika nusu fainali ya mashindano ya Afrika Mashariki baina ya shule za upili – FEASSA yanayoendelea mjini Kakamega.

Hii ni baada ya timu hizo kumaliza za kwanza na pili mtawalia kwenye makundi yao. Ngarambe hiyo yenye hisia mseto na ufuasi mkubwa itakuwa ya pili mwaka huu baada ya ile ya fainali ya kitaifa ambayo JOBO walishinda bao moja kwa sufuri.

Katika nusu fainali ya pili, washindi wa kundi B – Bukedea (UG) watakabana na Butere waliomaliza wa pili kwenye kundi A. Mechi hizo zitagaragazwa ugani Bukhungu kesho alhamisi.

Share This Article