Shule ya Archbishop Njenga yabanduliwa FEASSSA

Martin Mwanje
1 Min Read

Shule ya wasicha ya Archbishop Njenga leo Jumatano imebanduliwa kwenye mashindano ya michezo ya Afrika Mashariki baina ya shule za upili (FEASSSA) yanayoendelea mjini Kakamega. 

Hii ni baada ya kulazwa na Kawempe Muslim ya Uganda mabao manne kwa mawili katika nusu fainali.

Matokeo hayo yameizika ndoto ya waandalizi ya kunyakuwa taji hilo kwani pia wawakilishi wengine wa Kenya – Nasokol, Kobala, Madira na Butere walibanduliwa kwenye hatua ya makundi.

Katika nusu fainali ya pili, St.Noa pia ya Uganda waliwapiku Waganda wenzao – Amus College, goli moja kwa sufuri.

Fainali baina ya washindi hao itachezwa keshokutwa Ijumaa ugani Bukhungu

Share This Article