Senegal na Sudan wajaa robo fainali kipute cha CHAN

Sudan waliongoza kundi D  kwa alama 5 sawa baada ya kutoka sare tasa na Senegal waliomaliza nafasi ya pili kwa pointi sawa lakini wakiwa na uhaba wa magoli .

Dismas Otuke
0 Min Read

Mabingwa watetezi Senegal na Sudan,walikamilisha orodha ya timu nane zitakazocheza  kwota fainali za kindumbwendumbwe cha CHAN.

Sudan waliongoza kundi D  kwa alama 5 baada ya kutoka sare tasa na Senegal waliomaliza nafasi ya pili kwa pointi sawa lakini wakiwa na uhaba wa magoli.

Mechi hiyo ilipigwa uwanjani Amaan kisiwani Zanzibar jana usiku huku Nigeria ikiwazaba Congo 2-0 katika mchuano ulioandaliwa uwanjani Benjamin Mkapa.

Share This Article