Mvutano wa mgomo wa wauguzi Machakos

Martin Mwanje
1 Min Read

Wauguzi wanaoendelea na mgomo katika kaunti ya Machakos wameombwa kufanya mazungumzo ya makubaliano ya kurejea kazini ili kuokoa maelfu ya wananchi wanaokosa huduma za afya katika kaunti hiyo.

Akizungumza katika kanisa la Salvation Army Kithimani, Naibu Gavana wa Machakos Francis Mwangangi amemtaka kiongozi wa chama cha wauguzi tawi la Machakos Michael Saka kulegeza msimamo mkali wa kuendelea na mgomo huo na kuingia kwa meza ya mazungumzo na kukubali ahadi za malipo ambazo serikali ya kaunti ya Machakos imekubali kufikia sasa.

Mwangangi akikiri kwamba mgomo wa sasa umeathiri pakubwa utoaji wa huduma za afya katika kaunti hiyo na kuathiri maelfu ya wananchi wake na ipo haja ya mgomo huo kusitishwa mara moja.

Aidha, ameilaumu serikali kwa kukosa kutekeleza ugatuzi kikamilifu nchini na kusababisha mizozo kama ule wa sasa wa afya nchini kutokana na kutokuwepo kwa uwazi wa utendakazi na ufadhili wa kutosha.

Share This Article