Bongo na Madagascar zafuzu robo fainali ya CHAN

Madagascar waliomaliza nafasi ya tatu mwaka 2022 walimaliza katika nafasi ya pili kwa pointi 7 sawia na Mauritania,baada ya kuwachabanga Burkina Faso magoli 2-1 katika uwanja wa Amaan.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa fainali za kombe la CHAN,Tanzania maarufu kama Taifa Stars walijikatia tiketi kwa awamu ya kwota fainali baada ya kutwaa nafasi mbili za kwanza kundini B.

Taifa Stars walilazimishwa kwenda sare tasa dhidi ya Jamhuri ya afrika ya Kati, katika mchuano uliosakatwa Jumamosi usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Madagascar waliomaliza nafasi ya tatu mwaka 2022, walimaliza katika nafasi ya pili kwa pointi 7 sawia na Mauritania,baada ya kuwachabanga Burkina Faso magoli 2-1 katika uwanja wa Amaan.

Tanzania walimaliza mashindano bila kushindwa wakizoa alama 10 na watakuwa nyumbani Agosti 22 kwa kwota fainali.

Upande wao Madagascar watasafiri hadi Kenya kwa kwota fainali pia siku iyo hiyo.

Share This Article