Mshukiwa wa ujambazi akamatwa Kiambu

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa uhalifu akamatwa Kiambaa.

Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), wamemkamata mshukiwa wa uhalifu, anayedaiwa kuhusika katika visa vya ujambazi Rweno na Kiambaa kaunti ya Kiambu.

Kulingana na DCI kupitia ukurasa wa X, Stephen Igogo Kariuki mwenye umri wa miaka 26, alikamatwa akiwa katika maficho yake polisi walipotekeleza operesheni baada ya kupashwa habari na wananchi.

“Baada ya kukamatwa, mshukiwa huyo aliwapeleka maafisa wa polisi katika nyumba yake, na walipopekua, walipata bastola aina ya retay falcon,” ilisema DCI kwenye ukurasa wa X.

Maafisa hao walisema bastola hiyo huenda imetumika kutekeleza visa kadhaa vya uhalifu, na imewasilishwa katika maabara ya kitaifa kwa uchunguzi wa kisayansi.

Kwa sasa Kariuki  anazuiliwa katika korokoro za polisi, akisubiri kufunguliwa mashtaka mahakamani.

TAGGED:
Share This Article