Bei za lita moja ya mafuta ya Petroli na Mafuta Taa, zimepungua kwa shilingi moja, kulingana na bei mpya zilizotangazwa Alhamisi na Halmashauri ya kudhibiti Kawi na Petroli hapa Nchini (EPRA).
Katika bei hizo mpya, Jijini Nairobi, lita moja ya Petroli itauzwa shilingi 185.31, ile ya Diesel iuzwe shilingi 171.58 nayo lita moja ya Mafuta Taa itauzwa shilingi 155.58.
“Bei hizo zinajumuisha asilimia 16 ya ushuru wa VAT, kuambatana na sheria ya Fedha ya mwaka 2023…..” ilisema sehemu ya taarifa ya EPRA.
Jijini Mombasa, lita moja ya Petroli itauzwa shilingi 182.03, Diesel ikiuzwa shilingi 168.30, nayo lita moja ya Mafuta Taa ikuzwa shilingi 152.29.
Lita moja ya Petroli Kisumu itauzwa shilingi 185.16, Diesel shilingi 171.80 nayo Mafuta Taa shilingi 155.83.
Mnamo Julai 14,2025, EPRA iliongeza bei ya lita moja ya Petroli kwa shilingi 8.99, Diesel kwa shilinga 8.67 na Mafuta Taa kwa shilingi 9.65.