Wakenya watengewa maeneo ya kutazama mchuano wa Kenya na Zambia

Hii ni katika juhudi za kuzuia mashabiki kusongamana ndani ya uwanja wa Kasarani jinsi ilivyoshuhudiwa wiki jana katika ushindi wa bao moja kwa bila wa Kenya dhidi ya Morocco.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya michezo kwa ushirikiano na kamati andalizi ya fainali zinazoendelea za kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN), imetenga maeneo ambayo mashabiki watatazama mechi kati ya Kenya na Zambia Jumapili alasiri.

Maeneo hayo ambayo yatawekwa runinga kubwa yanajumuisha Uhuru Park, Lucky Summer, eneo la Ngomo nyuma ya uwanja wa Kasarani, Dandora Stadium, Utalii, Jacaranda Grounds na Kibera DC Grounds.

Hii ni katika juhudi za kuzuia mashabiki kusongamana ndani ya uwanja wa Kasarani jinsi ilivyoshuhudiwa wiki jana katika ushindi wa bao moja kwa bila wa Kenya dhidi ya Morocco.

Shirikisho la Kandanda Afrika tayari limetoza FKF, faini mara mbili na kutishia kutoa adhabu zaidi endapo utovu wa nidhamu utashuhudiwa katika mechi ya Jumapili.

Share This Article