Jitahadhari na wauzaji  tiketi ghushi za mechi ya Kenya na Zambia

Mitandano hiyo inadai kuwa tiketi zinauzwa kwa ada ya shilingi 200 na 500 kama tu zile Mookh.Com.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wauzaji wa tiketi bandia wamejitokeza baada ya kutangazwa kumalizika kwa tiketi halali za mechi ya kundi A kuwania kombe la CHAN kati ya Kenya na Zambia, Jumapili hii katika uwanja wa Kasarani.

Tiketi 27,000 zilizotengewa mechi hiyo kwa mashabiki zilimalizika mapema Jumatatu, chini ya saa mbili baada ya kampuni ya Mookh.com, kufungua uuzaji tiketi.

Hata hivyo, ipo mitandao mingi inawahadaa watu kuwa kuna tiketi 5,000 za ziada za mechi hiyo zinazouzwa.

Mitandano hiyo inadai kuwa tiketi zinauzwa kwa ada ya shilingi 200 na 500 kama tu zile Mookh.Com.

Kama njia ya kuhakikisha mashabiki wasio na tiketi hawataingia uwanjani Jumapili, Wizara ya Michezo imetenga maeneo sita ambayo mashabiki watatazama mechi kupitia kwa runinga.

Tahadhari usitapeliwe na kumbuka kuwa tiketi halali za CHAN zinauzwa na kampuni ya Mookh.com pekee.

Share This Article