FKF yapigwa faini ya shilingi milioni 6.5 kwa utovu wa usalama mechi ya Kenya na Morocco

Aidha, CAF imeonya kuwa huenda ikachukua hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya Kenya, ikiwemo kuhamishia mechi za Harambee Stars hadi ugenini endapo visa hivyo vitarudiwa katika mechi zijazo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la Kandanda Nchini (FKF), limepigwa faini ya shilingi milioni 6.5, kutokana na visa vya utovu wa usalama wakati wa mechi baina ya Kenya na Morocco, kuwania kombe la CHAN Jumapili iliyopita katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Bodi ya nidhamu ya shirikisho la soka barani CAF imeitoza FKF faini hiyo baada ya baadhi ya mashabiki kuvunja lango la kuingia Kasarani na polisi kushindwa kuthibiti umati.

Aidha, CAF imeonya kuwa huenda ikachukua hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya Kenya, ikiwemo kuhamishia mechi za Harambee Stars hadi ugenini endapo visa hivyo vitarudiwa katika mechi zijazo.

Share This Article