Mauritania itachuana na Burkina Faso leo katika mechi ya kundi B, huku mshindi akijiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali wakati timu itakayoshindwa ikiyaaga mashindano ya CHAN.
Mechi hiyo itapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia saa mbili usiku.
Awali Madagascar watakabana na Jamhuri ya Afrika ya Kati kuanzia saa kumi na moja jioni.
Madagascar watahitaji ushindi ili kuweka hai ndoto ya kufuzu kwa robo fainali wakiwa na alama moja baada ya mechi mbili.
Tanzania inaongoza kundi hilo kwa alama 9, baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza.
Mauritania wanakalia nafasi ya pili kwa alama 4, moja zaidi ya Burkina Faso.