CHAN 2024: Tiketi za mechi ya Kenya na Zambia zamalizika

Tiketi hizo zimepunguzwa kutoka 48,000 hadi 27,000, kutokana na utovu wa usalama ulioshuhudiwa katika mechi tatu za awali za Kenya.

Dismas Otuke
1 Min Read

Teketi 27,000 zilizotengewa mashabiki kwa mechi ya Kenya na Zambia Jumapili hii katika uwanja wa Kasarani zimemalizika.

Kampuni ya MOOKH iliyojukumiwa kuuza tiketi imekamilisha uuzaji wa tiketi hizo chini ya saa mbili baada ya kufungua uuzaji mapema leo Jumanne.

Tiketi hizo zimepunguzwa kutoka 48,000 hadi 27,000, kutokana na utovu wa usalama ulioshuhudiwa katika mechi tatu za awali za Kenya.

Kenya haina budi kuishinda Zambia Jumapili ili kuongoza kundi A, na kupata fursa ya kucheza robo fainali nyumbani.

Share This Article