Wakulima ukanda wa Pwani watakiwa kukumbatia kilimo cha kisasa

Martin Mwanje
1 Min Read

Huku mabadiliko ya tabia nchi yakiendelea kuathiri kiwango cha mvua, wakulima katika ukanda wa pwani wametakiwa kukumbatia ukulima wa kisasa ili kuimarisha mazao yao.

Akizungumza katika maonyesho ya kilimo biashara katika Chuo Kikuu cha Pwani, kaunti ya Kilifi, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Nafaka ukanda wa Afrika Mashariki Gerald Masila amewataka wakulima kuchangamkia matumizi ya pembejeo na teknolojia ili kupata mazao zaidi katika mashamba yao.

Wakati huo huo, Masila amewataka wakulima kupanda mimea inayostahimili mvua fupi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo, wakulima wameitaka serikali kuendeleza maonyesho hayo yanayosheheni kilimo darasa kila mwaka ili waweze kuelimika zaidi.

Maonyesho hayo yamewaleta pamoja wakulima zaidi ya elfu mbili kutoka kaunti mbalimbali za eneo la Pwani.

Share This Article