Wenyeji Kenya Harambee Stars watashuka dimbani Kasarani kuanzia saa tisa alasiri kwa mechi ya kundi A kuwania kombe la CHAN.
Harambee Stars wanaoongoz akundi A kwa alama 4 watahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya robo fainali wakati Morocco walio na alama 3 baada ya mechi moja pia wakiwinda ushindi, ili kuongeza matumaini ya kufuzu kwa kwota fainali.
Morocco waliishinda Angola magoli 2-0, katika mchuano wa ufunguzi wakati Kenya ikiwalemea DR Congo, bao moja kwa bila na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Angola.

Kenya ni sharti washinde mechi ya leo huku Morocco, wakiwa bado na uwezo wa kufuzu kwa mwondoano hata wakipoteza leo kwani watakuwa wamesaza mechi mbili dhidi ya Zambia na DRC.
Morocco na Kenya wanakutana kwa mara ya sita leo kwa jumla na mara ya kwanza katika CHAN, Atlas Lions wakishinda mechi tatu na kutoka sare michuano miwili.
Pambano la leo litarushwa mubasahara kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1.