Uganda Cranes kurejea Namboole leo dhidi ya Guinea

Mchuano huo utaanza kutifua vumbi saa mbili usiku huku wenyeji wakihitaji kurejelea tambo za ushindi baada ya kuambulia kichapo cha tatu bila dhidi ya Algeria

Dismas Otuke
1 Min Read

Waandalizi wenza wa fainali za kombe la Afrika kwa wanandinga wa ligi za nyumbani CHAN, Uganda Cranes, watarejea uwanjani Mandela leo jioni kwa mechi ya pili ya kundi C dhidi ya Guinea.

Mchuano huo utaanza kutifua vumbi saa mbili usiku huku wenyeji wakihitaji kurejelea tambo za ushindi baada ya kuambulia kichapo cha tatu bila dhidi ya Algeria katika mechi ya ufunguzi.

Upande wao Guinea wanastaka ushindi wa pili ili kukaribia kufuzu kwa robo fainali baada ya kuwashinda Niger goli moja bila jawabu katika mechi ya ufunguzi.

Share This Article