Trump na Putin kukutana katika siku zijazo, afisa wa Kremlin asema

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin wamekubaliana kukutana katika “siku zijazo”, msaidizi wa Kremlin amesema.

Inafuatia Trump kusema kulikuwa na “nafasi nzuri” anaweza kukutana na wenzake wa Urusi na Ukraine pamoja ana kwa ana “hivi karibuni sana” ili kujadili kumaliza vita nchini Ukraine.

Makataa ya Trump kwa Urusi kukubali kusitisha mapigano nchini Ukraine la sivyo itakabiliwa na vikwazo vikali zaidi inatamatika Ijumaa.

Mkutano unaowezekana kati ya Trump na Putin utafuatia mjumbe wa Marekani Steve Witkoff kufanya mazungumzo na rais wa Urusi siku ya Jumatano.

Witkoff amesafiri hadi Moscow mara nne hapo awali, ziara zikifuatiwa na matumaini kutoka kwa Trump lakini hatimaye hakuna mafanikio makubwa katika mazungumzo ya amani.

Share This Article