Aboud Omar asifia michuano ya CHAN, asema ni fursa nzuri kwa wachezaji kujitangaza

"Hiyo mita moja imetoa changamoto na kuinua morali kwa wachezaji kwenye kambi,na tutacheza na Angola tukiwa roho juu."akaongeza Omar

Dismas Otuke
1 Min Read

Nahodha wa Harambee Stars Aboud Omar, amesifia mashindano ya CHAN, akiyataja kuwa fursa bora kwa wachezaji wa humu nchini kujitangaza na kujiuza.

Akizungumza jana usiku kwenye mahojiano na Wanahabari jana usiku ,Omar alisema wachezaji haswa wanaoshiriki mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza wanapaswa kuwa makini kutokana na uwepo wa mawakala wanaotafuta wachezaji wa kusajili .

“CHAN  ni platform kubwa kwa wachezaji haswa wanaoshiriki mashindano ya kimataifa kwa mara ya kwanza,wachezaji wapaswa kujituma ili kupata soko kupitia haya mashindano,”akasema Omar

Nahodha huyo aidha alipongeza zawadi ya pesa waliyopewa na Rais William Ruto, akiongeza kuwa imeongeza morali kikosini kuelekea mechi ya leo dhidi ya Angola.

“Hiyo mita moja imetoa changamoto na kuinua morali kwa wachezaji kwenye kambi,na tutacheza na Angola tukiwa roho juu.”akaongeza Omar

Hata hivyo  Omar amekanusha kuwa pesa hizo walizituzwa na Rais huenda zikawatia mshawasha wachezaji na kukosa kumakinika katika mechi zijazo.

Harambee Stars itakabiliana na Angola leo usiku katika uwanja w akimataifa wa Kasarani katika mechi ya pili ya kundi A ,wenyeji wakihitaji ushindi  ili kuwa katika nafasi bora kufuzu kwa robo fainali.

 

Share This Article