Wabongo wanusia robo fainali ya CHAN kwa mara ya kwanza

Tanzania wanaongoza kundi hilo kwa alama sita, wakifuatwa na Burkina Faso kwa pointi 3 baada ya kuwagaragaza Afrika ya Kati magoli 4-2 katika mechi ya kwanza jana jioni

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa makala ya nane ya fainali za kombe la CHAN, Tanzania, wanakaribia kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza baada ya kusajili ushindi wa bao moja bila jibu jana usiku dhidi ya Mauritania.

Mchuano huo wa kundi B ulipigwa katika uga wa kitaifa wa Benjamin Mkapa jana usiku, bao pekee na ushindi kwa Taifa Stars likipachikwa kimiani na Shomari Kapombe kunako dakika ya 89, alipovurumiza kombora baada ya kupokea pasi ya Iddi Seleman.

Tanzania wanaongoza kundi hilo kwa alama sita, wakifuatwa na Burkina Faso kwa pointi 3, baada ya kuwagaragaza Afrika ya Kati magoli 4-2 katika mechi ya kwanza jana jioni

Share This Article