Mawaziri wawili wa Ghana wafariki kwenye ajali ya helikopta

Tom Mathinji
1 Min Read
Mawaziri wawili wa Ghana wafariki kwenye ajali ya helikopta.

Waziri wa Ulinzi wa Ghana na mwenzake wa Mazingira pamoja na watu wengine sita, wamefariki baada ya helikopta walimokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Ashanti, hayo yamethibitishwa na msemaji wa serikali ya nchi hiyo.

Waziri wa ulinzi Edward Omane Boamah na wa Mazingira, Sayansi na Teknolojia Ibrahim Murtala Muhammed, walifariki kwenye ajali hiyo, huku Mkuu wa Wafanyakazi Julius Debrah akitaja ajali hiyo kuwa janga la taifa.

Hapo awali Vikosi vya Ulinzi vya Ghana vilisema kuwa helikopta aina ya Z9 iliyokuwa na wafanyakazi watatu na abiaria watano ilitoweka kwenye rada.

Helikopta hiyo iliondoka Jijini Accra, saa tatu na dakika 12 saa za nchi hiyo, ikielekea mjini Obuasi katika hafla ya kukabiliana na uchimbaji haramu wa madini.

Maafisa wa nchi hiyo bado hawajathibitisha chanzo cha ajali hiyo, huku Mkuu huyo wa wafanyakazi akiagiza bendera kupeperushwa nusu mlingoti.

TAGGED:
Share This Article