Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) eneo la magharibi imemkamata Chifu Patrick Oyalo wa Lokesheni ya Marama Central, kaunti ya Kakamega kwa madai ya kuitisha hongo.
Chifu huyo anadaiwa kuitisha familia moja iliyofiwa shilingi elfu kumi kuwasaidia kupata stakabadhi ya kufanikisha kupata hatimiliki ya ardhi baada ya kifo cha baba yao.
Oyalo alitiwa mbaroni siku ya Jumanne baada ya kupatikana akiwa amepokea shilingi elfu nane za mlungula huo.
Anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Bungoma akisubiri kufikishwa mahakamani.