Maambukizi ya kifua kikuu kwa watoto yaibua wasiwasi Turkana

Tom Mathinji
1 Min Read
Kaunti ya Turkana inaimarisha juhudi za kukabiliana na Kifua Kikuu.

Kaunti ya Turkana inajizatiti kuimarisha vita dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) huku kiwango cha matibabu kikiwa ni asilimia 51.

Kiwango hicho ni cha chini ikilinganishwa na lengo la kitaifa la asilimia 90, wakati ambapo visa vya mambukizi ya ugonjwa huo kwa watoto vimeongezeka na kufikia asilimia 27.

Hii  ikiwa ni karibu mara mbili ya kiwango cha juu kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Kupitia ushirikiano na washirika wa kimaendeleo, kaunti hiyo inaboresha uchunguzi dhidi ya ugonjwa huo, matibabu na uhamasisho katika sehemu za mashinani ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.

Kwenye mkutano ulioungwa mkono na shirika la World Relief Kenya, ilibainika kwamba mpango unaofadhiliwa na hazina ya Global Fund utatoa matibabu bora kando na kuzuia maambukizi kwa wakazi wa Turkna.

Mpango huo unalenga wagonjwa kutoka sehemu za Loima, huko Turkana ya Kati,  Turkana Kaskazini, Turkana Kusini, Turkana Mashariki na Magharibi.

Naibu Mkurugenzi wa Afya ya Jamii Gabriel Lopodo alisema kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita, serikali ya kaunti hiyo ilikuwa imewekeza kwenye mitambo zaidi ya eksirei na mashine za GeneXpert ili kuboresha utambuzi wa mapema wa ugonjwa huo na hivyo kuimarisha utoaji matibabu ya ugonjwa wa TB.

TAGGED:
Share This Article