Uganda Cranes watafungua harakati za kuwania kombe la CHAN kundini C, watakapomenyana na Algeria katika uwanja wa Nelson Mandela (Namboole) mjini Kampala.
Mchuano huo utang’oa nanga saa mbili usiku ukitanguliwa na ule kati ya Niger na Guinea kuanzia saa kumi na moja usiku.
Timu nyingine kundini C ni Afrika Kusini.
Mataifa 19 yanashiriki kipute hicho kinachoandaliwa na mataifa matatu: Kenya, Uganda, na Tanzania.