Wenyeji wenza wa Makala ya nane ya kipute kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani, CHAN, Taifa Stars ya Tanzania, walifungua kipute cha mwaka huu kwa ushindi mkubwa wa 2-0, dhidi ya Burkina Faso kundini B Jumamosi usiku.
Tanzania waliotawala mchuano huo kutoka kipenga cha kwanza walichukua uongozi kunako dakika ya 3 ya mazidadi katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Abdul Hamisi Suleiman kupitia mkwaju wa penati.
Wakibebwa na hamerere na hamkani za mashabiki wa nyumbani katika furifuri ya uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa, Stars walizidisha mashambulizi. Mohammed Hussein aliongeza la pili dakika ya 71 baada ya kushirikiana vyema na Mutadhir Yahya kunako dakika ya 71.
Mechi hiyo ilianza rasmi saa mbili usiku baada ya sherehe za kufana za ufunguzi.
Wasanii kadhaa akiwemo Rayvanny walitumbuiza katika sherehe za ufunguzi.
Kinara wa shirikisho la soka barani Afrika Dkt. Patrice Motsepe alihudhuria pambano hilo.

Hatimaye baada ya subira ya muda, Afrika Mashariki inaandaa fainali za CHAN.
Ili kuweka hai matumaini ya kuingia hatua, Tanzanoa ni sharti waishinde Mauritania katika mechi ya pili Agosti.
Burkina Faso upande wo ni sharti waishinde Afrika ya Kati Juni 7 kwa mchuano wa pili.
CHAN itaingia siku ya pili, Kenya wakipambana kundini na mabingwa mara mbili DR Congo kuanzia saa tisa kabla ya Angola kushikana mashati na Morocco katika uwanja wa Nyayo saa kumi na mbili jioni.
Mauritania watahitimisha shughuli dhidi ya Madagascar saa mbili usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa.