Serikali itatimiza ahadi zake kwa Wakenya, asema Kindiki

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki asema serikali itatimiza ahadi zake.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amesema serikali ya Kenya Kwanza inajizatiti  kutekeleza na kukamilisha nusu ya ahadi zake kufikia mwisho wa muhula wake wa kwanza.

Akizungumza leo Ijumaa  katika shule ya upili ya wavulana ya Kabarnet wakati wa hafla ya mpango wa kuwawezesha wakazi wa Baringo ya kati, Prof. Kindiki, alisema amani inayopatikana katika kaunti ya Baringo imetokana na mkakati mpana wa serikali kuhusu usalama.

Aidha, alibainisha kuwa hali ya utulivu katika eneo hilo imefungua milango ya ukuaji katika sekta ya elimu, kilimo na afya.

Naibu huyo wa Rais alisema kuwa walimu 70,000 wameajiariwa huku serikali ikilenga kuwaajiri walimu laki moja kufikia mwaka 2026.

Kadhalika, alitangaza mpango wa ajira ya vijana kupitia mpango wa Kazi Mtaani, huku akisema miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na mpango wa afya ya umma imetoa nafasi za ajira ambao wakenya milioni 25 wamenufaika kote nchini.

Share This Article