EACC yatwaa ardhi ya Shirika la Reli Nchini iliyokuwa imenyakuliwa

Tom Mathinji
1 Min Read
EACC imetwaa ardhi ya Shirika la Reli Nchini iliyokuwa imenyakuliwa.

Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi hapa nchini (EACC), imetwaa ardhi ya shilingi Milioni 50 inayomilikiwa na Shirika la Reli Nchini katika kaunti Mombasa.

Kupitia kwa taarifa tume ya EACC ilisema ardhi hiyo ilitolewa kwa njia haramu kwa kampuni ya Kizingo Apartments Limited, kabla ya kuhamishwa kwa kampuni ya Kizingo Condominium Limited mwaka 2011.

Ardhi hiyo inayojulikana Mombasa/Block XXVI/1137 ina ukubwa wa hekari  0.0873.

Ardhi hiyo iko kwenye barabara ya Pwani, karibu na makutano ya barabara ya David Kayanda na iliyo na nyumba iliyojengwa na kampuni ya Reli ya Afrika Mashariki.

“Ardhi hiyo imekuwa chini ya Shirika la Reli Nchini tangu kuzinduliwa kwake,” ilisema taarifa hiyo.

Kufuatia uchunguzi wa EACC, kesi ya kutwaa ardhi hiyo iliwasilishwa Julai 7,2020 katika Mahakama ya kushughulikia masuala ya mazingira na ardhi kaunti ya Mombasa.

TAGGED:
Share This Article