NACADA yawatolea walevi kucha

Watakaoathiriwa ni waraibu wa pombe, wauzaji, na hata wasafirishaji.

Dismas Otuke
1 Min Read

Sheria mpya zilizopendekezwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Matumizi ya Pombe na Mihadarati (NACADA), zinatarajiwa kuathiri  wadau katika sekta hiyo.

Watakaoathiriwa ni waraibu wa pombe, wauzaji, na hata wasafirishaji.

NACADA inapendekeza kupiga marufuku uuzaji pombe katika maeneo ya umma ikiwemo kwenye ufukwe, barabara kuu, mashine za kuuza pombe, karibu na taasisi za elimu, ndani ya viwanja, mikahawa, mbuga, na vituo vya mafuta.

Aidha, NACADA inapendekeza kupigwa marufuku kwa matangazo ya pombe mitandanoni, uuzaji wa pombe kwenye mitandao, uchuuzi wa pombe, na usafirishaji wa pombe kama mzigo.

Mapendekezo mengine ni kupandisha umri wa kunywa pombe kuwa  miaka 21 kutoka miaka 18; wanaofanya matangazo ya pombe ni lazima wawe zaidi ya umri wa miaka 25; na pia magari ya kusafirisha pombe yataruhusiwa barabarani kati ya saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

Pia matangazo ya bei ya pombe yatapigwa marufuku.

Mapendekezo hayo endapo yatatekelezwa huenda yakawaacha kwenye njia panda wategemezi wa vileo kwa njia moja au nyingine wakiwemo wanywaji, wauzaji, wasafirishaji, na hata wamiliki wa baa, na pia ushuru unaokusanywa kupitia kwa vinywaji utapungua.

TAGGED:
Share This Article