Waziri wa michezo Salim Mvurya ameelezea kuridhishwa kwake na matayarisho yaliyofanywa katika uwanja wa Kasarani, kwa maandalizi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN kuanzia Jumamosi hii.
Waziri amepongeza ushirikiano baina ya kamati mbalimbali ikiongozwa na kamati andalizi kwa matayarisho kabambe yaliyofanywa Kasarani.
Harambee Stars itafungua dimba hilo la CHAN kwa mechi dhidi ya DR Congo Jumapili hii kuanzia saa tisa alasiri katika mchuano wa kundi A.
Mechi nyingine za kundi A kando na mechi nne za Harambee Stars zitasakatwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.
Kenya itaandaa mechi 12 za kipute hicho ikiwemo fainali ya Agosti 30.
Wenyeji wenza Tanzania wataandaa mchuano wa ufunguzi kundini B Jumamosi hii dhidi ya Burkina Faso kiwarani Benjamin Mkapa.